Klabu ya soka ya Manchester United imemtangaza Mholanzi, Louis van Gaal kuwa kocha wake mkuu baada ya kumtimua mwezi uliopita David Moyes.
Van Gaal ataanza kazi rasmi ya kuinoa Manchester mara baada ya kumalizika kwa fainali za kombe la Dunia nchini Brazil ambako atakuwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Uholanzi.
Man U na kocha huyo wameingia mkataba wa miaka mitatu huku Mholanzi huyo akisema ni furaha kwake kufundisha timu kubwa Duniani.
Ryan Giggs aliyekuwa kocha wa muda wa timu hiyo, atakuwa kocha msaidizi wa Van Gaal.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni