.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 19 Mei 2014

MAKUNDI YA KIMATAIFA YATAKA UDHIBITI WA CHAKULA KAMA ILIVYO KWA TUMBAKU

Makundi ya Kimataifa yametaka sekta ya chakula kudhibitiwa kama ilivyo kwa zao la tumbaku, kutokana na tatizo la unene kuwa na athari kubwa zaidi duniani kuliko hata uvutaji wa sigara.

Shirika la Walaji Kimataifa pamoja na Shirikisho la Kukabiliana na Unene Duniani wametaka kuwepo kwa sheria kali za udhibiti wa utengenezaji vyakula.

Katika mapendekezo hayo wametaka vifungashio vya vyakula kuwa na picha zinazoonyesha madhara ya unene kwa mlaji, kama ilivyo kwenye pakiti za sigara.

Taasisi hizo zimesema vifo vinavyotokana na unene na kuwa na uzito mkubwa kupindukia vimeongezeka na kutoka watu milioni 2.6 mwaka 2005 hadi kufikia watu milioni 3.4 mwaka 2010.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni