Mshindi wa kwanza katika shindano la Nice & Lovely Miss Tanga 2014 kuondoka na gari dogo la kifahari aina ya Vitz.
Mkurugenzi wa kampuni ya Mac D Promotions, Irene Rweyunga ambao ndio waandaaji wa shindano hilo, amesema kuwa wamejidhatiti kulifanya shindano hilo kuwa la aina yake mwaka huu.
Irene amewataka warembo wenye vigezo kujitokeza sasa kuchukua fomu za ushiriki kwani mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni June 08' 2014. Fomu zinapatika Mkonge Hotel, Tanga Beach Resort, Danny Fashion, Sophia Records, Mwambao Fm, Ofisi za The Guardian Tanga, Breeze Fm, Nyumbani Hotel, Five Brothers, Yolanda Salon na D-Boutique
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni