Wanajeshi wawili wa Kikosi cha
Ulinzi cha Kenya (KDF) wamepigwa risasi na kufa katika shambulio
lililofanywa na wapiganaji wanaoshukiwa kuwa wa al Shabaab katika
eneo la Kiunga, huko Lamu kwenye mpaka wa Kenya na Somalia.
Wanajeshi hao walijibu mashambulizi
na kufanikiwa kumuua mmoja wa washambuliaji huku wengine wakifanikiwa
kutoroka kwenye tukio hilo lililotokea jumapili jioni, ambapo
wanajeshi wengine wawili walijeruhiwa.
Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Kenya,
limesema wanajeshi hao walikuwa kwenye gari aina ya Land rover
wakipita eneo la Milimani na ndipo gari lao lilipokwama kwenye tope
na walipokuwa wakijaribu kulisukuma gari lingine lilifika na kuanza
kuwashambulia kwa risasi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni