Idadi ya watu waliofikishwa hospitali mjini Songea mkoani Ruvuma kutokana na kunywa pombe aina ya Togwa inayosadikiwa kuwa na sumu sasa imefikia 325.
Taarifa toka mkoani humo zinasema kuwa, idadi hiyo imeongezeka leo kutokana na wagonjwa zaidi wanaoharisha na kutapika kufikishwa katika hospitali ya misheni Peramiho na zahanati ya Lyangweni na baadhi yao wakiwa na hali mbaya.
Watu hao walikumbwa na mkasa huo wakiwa katika sherehe ya kipaimara iliyoandaliwa na mkazi mmoja wa mjini Songea.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni