Timu ya madaktari wa Jamhuri ya Dominica imelazimika kukimbilia kwenye ndege moja iliyokuwa ikitoka Philadelphia baada ya mwanaume mmoja kupiga chafya na kupiga mayowe huku akisema ninaugua Ebola.
Abiria huyo raia wa Marekani ambaye alikuwa haugui Ebola alishikiliwa na maafisa wanne wa afya na kupelekwa kwenye kituo cha afya kilichopo uwanja wa ndege cha Punta Cana ambapo ilibainika hatokei Afrika.
Abiria wengine 255 walilazimika kukaa ndani ya ndege kwa muda wa saa mbili hadi hapo ilipobainika kuwa mtu huyo haugui Ebola, huku watumishi wa ndege hiyo wakisisitiza walikuwa wanaamini kuwa ulikuwa ni utani.
Hata hivyo baadaye iligundulika kuwa abiria huyo raia wa Marekani hakuwa na maambukizi ya ugonjwa huo, na passport yake kuonyesha kuwa hakuwahi kusafiri hata siku moja katika nchi za Afrika.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni