.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 11 Oktoba 2014

FAINALI ZA MATAIFA AFRIKA 2015 HATARINI KUPIGWA KALENDA KISA TISHIO LA EBOLA

Wenyeji wa Fainali za kombe la Mataifa Afrika mwaka 2015 nchi ya Morocco imeomba kusogezwa mbele kwa fainali hizo kufuatia tishio la maambukizi ya ugonjwa wa Ebola unaoenea kwa kasi katika nchi za Afrika Magharibi. 

Fainali hizo zimepangwa kuanza kati ya January 17 hadi February 08' 2015. 

Maombi ya kusogezwa mbele kwa fainali hizo yamewasilishwa kwa Shirikisho la Soka Barani Afrika ( CAF ). 

Zaidi ya watu 4,000 wamefariki dunia mpaka kufikia sasa katika nchi za Afrika Magharibi kutokana na ugonjwa wa Ebola. Nchi zilizoathirika zaidi ni Guinea, Liberia na Sierra Leone.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni