Katika mchezo huo, wenyeji walionekana kuonana zaidi na kucheza kitimu na kujikuta wanamaliza dakika 90 wakiwa na ushindi huo mnono ulifufua matumaini ya mashabiki wa soka wa Uingereza ambao hawana imani sana na timu yao katika michuano ya kimataifa.
Mabao ya Uingereza yaliwekwa kimiani na wachezaji Phil Jagielka aliyefunga bao la kwanza katika dakika ya 24, bao la pili likafungwa na Wayne Rooney kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 43.
Mabao ya Uingereza yaliwekwa kimiani na wachezaji Phil Jagielka aliyefunga bao la kwanza katika dakika ya 24, bao la pili likafungwa na Wayne Rooney kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 43.
Bao la tatu liliwekwa kimiani na mshambuliaji mwenye kasi sana uwanjani Danny Welbeck katika dakika ya 49, bao la nne lilifungwa na Andros Townsend 72, wakati bao la tano likiwekwa kimiani na beki wa San Marino Allesandro Della Valle katika dakika ya 78 wakati akiwa katika harakati za kuokoa.
Matokeo mengine ya mechi zilizochezwa jana usiku za kuwania kufuzu kwa Euro 2016:-
Sweeden 1 vs 1 Urusi
Slovakia 2 vs 1 Hispania
Slovenia 1 vs 0 Uswisi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni