.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 7 Oktoba 2014

MAMIA YA WAOMBOLEZAJI WAMSINDIKIZA MAREHEMU GLADNESS SEMGOJA KATIKA MAKAZI YAKE YA MILELE

Marehemu Gladness Semgoja. 

Mamia ya waombolezaji jana walijitokeza kwa wingi katika misa na baadaye maziko ya marehemu Gladness Semgoja ( 31 ) aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam. 

Marehemu Gladness alizikwa katika makaburi ya Agape Mbezi Kibanda cha Mkaa. 

Marehemu alikuwa afunge pingu za maisha na mchumba wake Adonia Barashikwa mwishoni mwa wiki hii, na kesho kutwa alhamisi 09 Octoba 2014 ilikuwa ifanyike sherehe ya kumuaga ( Send Off ). 

Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.
Mama mzazi wa marehemu, Janeth Chammafwa ( aliyekaa katikati ) akifarijiwa wakati wa maziko ya mtoto wake Gladness hapo jana.
Mama mzazi wa marehemu, Janeth Chammafwa akisaidiwa kuweka shada la maua katika kaburi la mtoto wake mpendwa Gladness Semgoja.
Mume mtarajiwa wa marehemu Gladness Semgoja, Adonia Barashikwa ( aliyevaa suti nyeusi na miwani ) akitoka kuweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa mke wake mtarajiwa.
Dada wa marehemu, Irene Mattle akisaidiwa na mume wake Patric Mattle kuweka shada la maua katika kaburi la mdogo wake, marehemu Gladness Semgoja.
Waombolezaji wakiwa makaburini.
Waombolezaji wakiwa makaburini.
Deogratius Rweyunga ( kushoto ) akishauriana jambo na shemeji wa marehemu, Patric Mattle baada ya kumaliza shughuli za mazishi.
                                                                         Waombolezaji wakiwa makaburini.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni