Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar
Pistorius alikuwa ni mtu aliyevunjika moyo baada ya kumuua mpenzi
wake Reeva Steenkamp, mwanasaikolojia wake ameieleza mahakama hii
leo.
Akiotoa maelezo yake mwanasaikolojia
wake Lore Hartzenberg ameseme Pisorius alikuwa ni mtu aliyevunjika
moyo na alikuwa akikatiza mazungumzo yao kwa kulia mara kwa mara.
Hata hivyo Mwendesha Mashtaka Gerrie
Nel amemtuhumu mwanasaikolojia huyo kwa kujaribu kulikwepa swali kuwa
Pistorius alikuwa amepata mpenzi mpya wakati bado akiwa na Steenkamp.
Pistorius anakabiliwa na kifungo cha
jela cha miaka 15, ingawa Jaji Masipa anaweza kutotoa adhabu hiyo na
badala yake amtake alipe faini.
Oscar Pistorius akiwa amekumbatiana na mwanamke ambaye hajafahamika
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni