.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 10 Oktoba 2014

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI TABORA

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzan Kaganda akiongea na waandishi leo tarehe 09.10.2014

                           TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 09/10/2014.

Ndugu waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, hapa mkoani kwetu Tabora kumetokea tukio lifuatalo

AJALI YA PIKIPIKI KUMGONGA MPANDA BAISKEL NA KUSABABISHA MAJERUHI:- 

Mnamo tarehe 09/10/2014 majira ya saa 12:40hrs eneo la stendi mpya ya basi Tabora askari wa mtu aliyefahamika KELVIN AFWILILE MWAKATOBE 25yrs akiwa anaendesha pikipiki alimgonga mwendesha baiskeli. 

Mara moja alikamatwa na na askari wa usalama barabarani na kumtaka mtuhumiwa aende kituo cha polisi baaada ya marumbano kijana huyo alimshambuliwa kwa makofi na kumpora kofia yake ya polisi na kutupa kitendo kilichofanya askari huyo kuita msaada na kuweza kumkamata BW. KELVIN kukamatwakwake kulisabisha wananchi wengi hususani madereva boda boda wakaandamana kwenda kituo cha polisi kati Tabora kwa nia ya kumkomboa mtuhumiwa huyo.

Kufuatia sakata hilo OCD kituo cha polisi kati aliamuru wakusanyikaji watawajike lakini walizidi kikisogelea kituo hicho ndipo askari polisi wakalazimika kutumia mabomu ya moshi na maji ya kuwasha kutawanya watu waliokuwa wanasogelea kituo na kufanikiwa kukamata watu 15 wakiwemo waendesha boda boda ambao walikuwa wanaongoza mgomo.

Ulizi iliimaralishwa katika kituo cha polisi na maeneo mengine na hali ya mkoa iko shwali.

                                                                         SUZAN S. KAGANDA –ACP.

                                                       KAMANDA WA POLISI MKOA WA TABORA

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni