Naibu katibu mkuu wizara ya habari,vijana,utamaduni na michezo Profesa Elisante Ole Gabriel katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwenye Uzinduzi wa Uhuru Marathon 2014 ambapo mbio hizo zitafanyika Leaders Club Jijini Dar es salaam tarehe 07/12/2014 kulia ni mratibu wa mbio hizo Innocent Melleck na kushoto ni mwenyekiti wa chama cha Riadha Dar Es Salaam Zainab Mbiro.
.Mratibu wa Uhuru Marathon Innocent Melleck akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa mbio hizo mwaka huu ambapo zitafanyika 07/12/2014 kwenye viwanja vya leaders Club jijini Dar Es Salaam kulia kwake ni Naibu Katibu mkuu wa wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na michezo Profesa Elisante Ole Gabriel.
Na Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya mbio nefu za Uhuru Marathon ambayo yamepangwa kufanyika Desemba 7 mwaka huu yamezinduliwa rasmi jana jijini Dar es Salaam kwa kuwataka wanariadha kujitokeza ili kuimarisha Amani,afya, uhuru, uzalendo na muungano wa Watanzania.
Akizungumza jana jijini, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof Olisante Ole Gabriel , alisema kuwa anaipongeza Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo kwa sababu zinalengo la kihistoria la kumbukumbu za Uhuru wa Tanzania.

Prof Elisante aliwaomba wahisani mbalimbali kujitokeza kwa wingi na kudhamini mbio hizo huku akisisitiza kuwa serikali ipo bega kwa bega katika kuhakikisha ujumbe wa mwaka huu unawafikia walengwa ambao ni jamii nzima ya kitanzania na wapenda amani wote ulimwenguni
Ndugu zangu serikali inawaomba kwa dhati kabisa watu na mashirika mbalimbali ya kiserikali na mashirika binafsi kujitokeza kwa wingi katika kudhamini mbio hizi kwa kuwa lengo lake ni chanya kwa taifa letu,hata pale serikali itakapohitajika kutoa ushirikiano wowote basi kama serikali tupo tayari kwa hilo muda wowote ,
Alisema kuwa kupitia mbio hizo suala la Amani litasisitiza na hakuna mahali popote duniani ambapo wananchi wake hawapendi Amani.
Alisema kuwa kupitia mbio hizo suala la Amani litasisitiza na hakuna mahali popote duniani ambapo wananchi wake hawapendi Amani.
“Mbio hizi zinafanyika huku jambo muhimu likiwa ni kusisitiza na kuuenzi Muungano wetu katika jamii iliyostahamilivu,” alisema kiongozi huyo wa wizara.
Aliwataka pia wenyeji wa mbio hizo, Chama cha Riadha mkoa wa Dar es Salaam (DAAA) kusimamia kikamilifu mbio hizo kwa sababu ni sehemu ya kuwaandaa wanariadha na mashindano mengine ya kimataifa watakayoshiriki.
Mratibu wa mbio hizo, Innocent Melleck, alisema kuwa mbali na kuendeleza vipaji vya wanariadha, mbio za Uhuru Marathon zina lengo la kuhamasisha Amani, umoja na mshikamano wa wananchi wa Tanzania.
Melleck alisema kuwa kupitia mbio hizo pia wananchi watashiriki kusisitiza Muungano uliopo hapa nchini.
Alisema kuwa anaamini mbio za mwaka huu zitasaidia kuutangaza mchezo wa riadha ambao miaka ya nyuma uliipa sifa kubwa Tanzania kwa wanariadha wake kupata medali katika mashindano ya kimataifa.
Aliongeza kuwa katika mbio hizo, wanariadha watachuana katika marathoni, nusu marathoni na mbio maalumu za kujifirahisha za kilomita tano.
Melleck aliitaja kauli mbiu ya mbio za mwaka huu ambazo zitaanzia kwenye viwanja vya Leaders jijini ni “ Uhuru Wetu, Amani Yetu, Tuitunze”
Naye Katibu Msaidizi wa DAAA, Ombeni Zavalla, alisema kuwa chama hicho kiko tayari kushirikiana na Kamati ya Maandalizi ili kufanikisha mbio hizo zinafanyika kwa kufuata taratibu zote za kiufundi.

Mbio za uhurumarathon zinafanyika kwa mwaka wa pili mfululizo hapa nchini ambapo mwaka jana zilifanyika tarehe 08/12/2013 hapa jijini Dar Es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Mohamed Gharib Bilal ambapo jumla ya wanariadha 2618 walishiriki mbio hizo toka katika mataifa 21
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni