Baada ya kushuhudia mechi kadhaa za michuano ya fainali za kombe la Mataifa ya Afrika, leo fainali hizo zinazofanyika nchini Equatorial Guinea zinaendelea kwa michezo ya kundi D.
Katika mechi za leo, Ivory Coast wanateremka dimbani kucheza na Guinea wakati mchezo mwingine wa kundi hilo utazikutanisha Mali na Cameroon.
Mchezo kati ya Ivory Coast na Guinea utachezwa katika uwanja wa Estadio de Malabo, ambapo nahodha wa Guinea Kamili Zeyatte uhenda asicheze mchezo huo kutokana na majeraha ya mguu na hakufanya mazoezi pamoja na wachezaji wenzake.
Ivory Coast itashuka dimbani chini ya nahodha wake Yaya Toure.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni