Simba wa milima ya Teranga, Senegal wameshindwa kutamba mbele ya Algeria baada ya kushuhudia timu hiyo ikifungwa jumla ya mabao 2-0 katika mchezo wa kundi C wa kukamilisha ratiba ya makundi katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Mataifa Afrika.
Algeria ambao wamemaliza wakiwa nafasi ya pili katika kundi hilo wamefikisha pointi 6 sawa na Ghana wanaoongoza kundi lakini wakitofautiana mabao ya kufunga.
Algeria sasa wameungana na Ghana kusonga mbele hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Mabao ya Algeria yaliwekwa kimiani na RiyadMahrez dakika ya 11 na bao la pili likafungwa na NabilBentaleb katika dakika ya 82
Mashabiki wa Algeria wakifurahia kufuzu kwa timu yao hatua ya robo fainali.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni