.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 18 Januari 2015

BALOZI SEIF AKAGUA UCHIMBAJI WA KISIMA MUEMBE MAJOGOO - JIMBO LA KITOPE

Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi aliyevaa shati rangi ya Kijani akikagua maendeleo ya uchimbaji wa Kisima cha maji safi katika Kijiji cha Muembe Majogoo.
Wanachama wa CCM na Wananchi wa Kijiji cha Muembe Majogoo wakiwa katika mkutano wa kutathmini suala la huduma za maji safi katika Kijiji chao wao na Mbunge wao Balozi Seif hayupo pichani hapo kwenye Tawi la CCM Muembe Majogoo.
Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kitope Mama Asha Suleiman Iddi akiwapa matumaini ya upatikanaji wa huduma za maji Sadfi na salama wananachi wa Kijiji cha Muembe Majogoo

                                                                          Na Othman Khamis Ame, OMPR

Uongozi wa Jimbo la Kitope uko katika jitihada za kufanya maarifa ya kuhakikisha huduma za maji safi na salama inapatikana katika kijiji cha Muembe Majogoo ili kuwaondoshea u Wananchi wa Kijiji hicho usumbufu wa ukosefu wa huduma hiyo muhimu.


Mbunge wa Jimbo la Kitope ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wanakati akizungumza na wanachama wa chama cha Mapinduzi pamoja na wananchi wa Muembe Majogoo mara baada ya kukagua shughuli za uchimbaji wa kisima katika kijiji hicho.

Balozi Seif alisema uongozi wa Jimbo hilo unaelewa vyema shida na matatizo yanayowakumba wananchi hao katika kutafuta huduma za maji safi na salama kwa muda mrefu. Hivyo kazi inayoendelea ya uchimaji wa kisima hicho imelenga kukabiliana na tatizo hilo.

Aliwahakikishia wananchi hao wa Kijiji cha Muembe Majogoo kwamba kazi hiyo ya uchimbaji wa kisima inayoendelea itakwenda sambamba na ununuzi wa mipira ya kusambazia maji katika kijiji hicho.

Aliwapongeza wanachama wa chama cha Mapinduzi na Wananchi wa Kijiji cha Muembe Majogoo kwa ustahamilivu wao wa muda mrefu waliouonyesha katika kipindi choche cha ukosefu wa huduma hiyo muhimu.

Akigusia suala la Kura ya maoni kuhusu Katiba Mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayopendekezwa pamoja na uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu Balozi Seif alisema Umoja na Amani Nchini Tanzania utadumu endapo Muungano uliopo hivi sasa utaendelea kuwepo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni