Bunge la Haiti limevunjwa baada ya
kushindwa kuafikiana katika majadiliano ya sheria mpya ya uchaguzi
nchini humo.
Rais wa Haiti Michel Martelly
amekuwa akijaribu kutafuta kuungwa mkono na Marekani, katika mpango
wake wa kuhairisha uchaguzi mkuu tena.
Wapinzani wake wamesema wataendelea
na maandamano mitaani yaliyodumu kwa miezi kadhaa katika kumshinikiza
rais huyo ajiuzulu ambaye kwa sasa anatawala kwa kutumia nguvu ya
sheria aliyonayo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni