Timu za soka za Chelsea na Liverpool zimetoka uwanjani bila kupata mshindi katika mchezo wa kuwania kombe la Capital One nchini Uingereza usiku wa kuamkia leo.
Katika mchezo huo uliomalizika kwa timu hizo kufungana bao 1-1, Chelsea ndio waliokuwa wa kwanza kupata goli lililofungwa kwa njia ya penati na mshambuliaji Eden Hazard katika dakika ya 18 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
Raheem Sterling akiisawazishia Liverpool. Kipindi cha pili Liverpool walirejea uwanjani kwa kishindo na kufanya mashambulizi langoni mwa Chelsea na hatimaye kufanikiwa kusawazisha goli hilo, baada ya mshambuliaji wake mwenye kasi Raheem Sterling kumtungua kipa wa Chelsea, Courtois katika dakika ya 59.
Timu hizo zitarudiana jumanne ya wiki ijayo, January 27' 2015
Raheem Sterling akiisawazishia Liverpool. Kipindi cha pili Liverpool walirejea uwanjani kwa kishindo na kufanya mashambulizi langoni mwa Chelsea na hatimaye kufanikiwa kusawazisha goli hilo, baada ya mshambuliaji wake mwenye kasi Raheem Sterling kumtungua kipa wa Chelsea, Courtois katika dakika ya 59.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni