.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 20 Januari 2015

FAINALI ZA MATAIFA AFRIKA 2015, BAFANA BAFANA YAKUMBANA NA KIPIGO TOKA KWA ALGERIA

Timu ya soka ya taifa ya Afrika Kusini, Bafana Bafana imekiona cha moto katika michuano ya kuwania kombe la Mataifa Afrika, baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 toka Algeria. 

Katika mchezo huo wa kundi C wa fainali hizo zinazofanyika nchini Equatorial Guinea, Algeria walionekana kuwazidi maarifa uwanjani Bafana Bafana na kuweza kupata ushindi huo ambao sasa unawanfanya waliongoze kundi lao.
Hata hivyo Afrika Kusini ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika kipindi cha pili dakika ya 51, bao likifungwa na Thuso Phala. 

Algeria walisawazisha bao hilo katika dakika ya 67 baada ya Thulan Hlatshwayo wa Afrika Kusini kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa. 

Bao la pili nala tatu yaliwekwa kimiani na wachezaji Faouzi Ghoulam dakika ya 72′ na Slimani katika dakika ya 83′.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni