Timu ya soka ya taifa ya Ghana jana ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Algeria katika mchezo wa kundi C wa kuwania kombe la Mataifa Afrika, fainali ambazo zinaendelea nchini Equatorial Guinea.
Katika mchezo huo, Ghana ilibidi wasubiri hadi dakika za majeruhi ndipo mshambuliaji wake mahiri Asamoah Gyan alipoifungia bao hilo muhimu katika dakika ya 90 ya mchezo.
Kwa matokeo hayo, Ghana ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 3 nyuma ya Senegal yenye pointi 4 ikiwa ndio kinara wa kundi C.
Nafasi ya tatu wapo Algeria wakiwa na pointi 3 na mkiani wapo Afrika Kusini wenye pointi 1.
Kocha wa Ghana, Avram Grant akimpongeza Asamoah Gyan baada ya kuifungia timu yake bao muhimu dhid ya Algeria hiyo jana.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni