.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 21 Januari 2015

FAINALI ZA MATAIFA AFRIKA 2015, MALI NA CAMEROON HAKUNA MBABE

Mali na Cameroon zimetoka uwanjani bila kumpata mshindi katika mchezo wa kundi D wa kuwania kombe la Mataifa ya Afrika ( Afcon 2015 ) zinazoendelea kuunguruma nchini Equatorial Guinea. 

Katika mchezo huo wa jana usiku, timu hizo zilijikuta zikifungana bao 1-1 na kulifanya kundi hilo kuwa gumu, kwani Ivory Coast na Guinea nazo zilifungana bao 1-1.
Mali ndio waliokuwa wa kwanza kutikisa nyavu za Cameroon katika dakika ya 71 kwa bao la Sambou Yabatare na kunako dakika ya 84 Cameroon walifanikiwa kusawazisha bao hilo lililofungwa na Onyongo Bitolo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni