.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 24 Januari 2015

FAINALI ZA MATAIFA AFRIKA 2015, SENEGAL NA AFRIKA KUSINI WAGAWANA POINTI

Simba wa milima ya Teranga, Senegal walipigana kufa na kupona na kufanikiwa kusawazisha bao walilokuwa wametanguliwa kufungwa na Afrika Kusini katika mchezo wa kundi C wa fainali za Mataifa ya Afrika zinazoendelea kuunguruma nchini Equatorial Guinea. 

Katika mchezo huo, Oupa Manyisa aliipatia Afrika Kusini bao katika dakika ya 47, lakini Senegal walikuja juu na kufanikiwa kusawazisha bao hilo katika dakika ya 60 mfungaji akiwa ni Kara Mbodji. 

Fainali hizo zitaendelea leo kwa michezo ya kundi D, ambapo Ivory Coast watashuka dimbani kucheza na Mali na kufuatiwa na mchezo mwingine kati ya Cameroon na Guinea.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni