Katika mchezo huo, Zambia ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 59 ya kipindi cha pili, bao lililofungwa na Emmanuel Mayuka.
Timu zote zilionekana kutandaza soka safi na Zambia kuwa wanafanya mashambulizi ya kushtukiza langoni mwa Tunisia.
Hata hivyo dakika ya 70 Tunisia walifanikiwa kupata bao la kusawazisha likifungwa na Ahmed Akaichi na baadaye Yasine Chikhaoui akaipatia Tunisa bao la pili nala ushindi katika dakika ya 88.
Kwa matokeo hayo Tunisia ndio vinara wa kundi hilo wakiwa na pointi 4.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni