Waziri wa Nishati na Madini, Mh Sospeter Muhongo hatimaye ametangaza rasmi kujiuzulu wadhifa wake hii leo kufuatia sakata la akaunti ya Tegeta Escrow.
Mh Muhongo ametangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya wizara hiyo.
Kujiuzulu kwa Mh Muhongo, kunafuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema aliyejiuzulu kutokana na sakata hilo, pamoja na aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Mh Anna Tibaijuka ambaye nafasi yake ilitenguliwa na Rais kufuatia sakata hilo hilo la Escrow.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni