.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 28 Januari 2015

JOSE MOURINHO ALIMWAA FAINI YA PAUNDI 25,000 KUTOKANA NA MATAMSHI YAKE

Shirikisho la soka nchini Uingereza ( FA ) limempiga faini ya paundi 25,000 kocha mkuu wa timu ya soka ya Chelsea, Mreno Jose Mourinho ( pichani ) baada ya kusema kuwa kuna kampeni kali dhidi ya timu yake inayofanywa na waamuzi uwanjani. 

Mourinho alitoa kauli hiyo Desemba 28'2014 wakati timu yake ilipotoka sare ya kufungana bao 1-1 na Southampton katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza, na kudai kuwa kuna kampeni ya kuhakikisha Chelsea haitwai ubingwa wa ligi kuu. 

Mbali ya kumpiga faini hiyo, FA pia imempa onyo kocha huyo msema hovyo.
NI KAMA ANASEMA!! Hawa hawanijui, nitawavuruga kwa maneno yangu ya kuudhi subiri.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni