.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 19 Januari 2015

LIGI KUU UINGEREZA, ARSENAL WAWANYAMAZISHA MANCHESTER CITY ETIHAD STADIUM

Timu ya soka ya Arsenal ikicheza ugenini katika uwanja wa Etihad jana imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mabingwa watetezi wa kombe la ligi kuu nchini Uingereza, Manchester City.
Katika mchezo huo uliokuwa mkali nawa kusisimua, Arsenal walijipatia bao la kwanza kwa mkwaju wa penati iliyowekwa kimiani na Santi Cazorla katika dakika ya 24. 

Penati hiyo ilitokana na nahodha na beki wa Manchester City, Vicent Kompany kumchezea madhambi Nacho Monreal ndani ya eneo la hatari. 

Bao la pili la Arsenal lilifungwa na Olivier Giroud katika dakika ya 67 na kuizamisha kabisa Manchester City.
Kwa matokeo hayo, Arsenal wamefikisha pointi 39 wakiwa nafasi ya tano, huku Manchester City wakiendelea kubaki nafasi ya pili wakiwa na pointi 47, pointi 5 nyuma ya vinara wa ligi hiyo Chelsea.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni