Mawaziri hao kwa pamoja waliongozana na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mheshimiwa Bw.Philip Malmo.
Katika mkutano huo mawaziri hao wote walielezea jinsi Wizara zao zinavyofanya kazi kuhakikisha kuwa huduma za afya zinawafikia walio wengi na pia kuhakikisha siku za usoni kila mtanzania atatanufaika na huduma hizo kwa kutumia bima ya afya bila kujali tofouti za uwezo wa vipato vyao.
Watanzania waishio Ujerumani wamefarajika sana na mkutano huo pia mawaziri wamewataka watanzania waishio ughaibuni kuchangia kuwekeza katika sekta ya huduma ya afya hata ikiwa ni sekta binafsi.
Mawaziri hao wamesema milango ya wizara zao hipo wazi kwa watanzania wanaotaka ushauri,ushirikiano au kuwekeza katika sekta hizo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni