.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 28 Januari 2015

MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA NCHINI APANDISHWA KIZIMBANI DODOMA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja amefikishwa leo katika mahakama ya Wilaya ya Dodoma akikabiliwa na mashtaka mawili ya kuwachochea wafanya biashara wa mkoa wa Dodoma kutenda kosa na kuwazuia wafanyabiashara hao kulipa kodi kwa kutumia mashine za kieletroniki za Efds.

Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama ya Mkoa wa Dodoma, Rebeka Mbilu, mwendesha mashtaka wa serikali Godfrey Wambali ameiambia mahakama hiyo kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Septemba 6, mwaka jana katika ukumbi wa chuo cha mipango kilichopo Mjini hapa.

Wambali amesema katika kosa la kwanza mshtakiwa alitenda kosa la jinai kinyume na kifungu cha sheria namba 390 kinachokwenda sambamba na kifungu cha 35 cha kanuni za adhabu sura ya 16.
Ambapo katika kosa la pili mshatakiwa alitenda kosa kinyume na sheria kifungu cha 107c cha sheria ya kodi sura ya 332 ya mwaka 2014.

Hata hivyo mshtakiwa alikana makosa yote mawili na alirudishwa rumande baada ya kukosa wadhamini wawili ambao walitakiwa kuwa na dhamana ya mali ya sh. 4 milion za mali zisizohamishika ikiwa ni pamoja na mmoja wa wadhamini hao kuwa ni mfanyakazi wa serikali.

Baada ya kushindwa kutimiza masharti hayo, Hakimu Mbilu aliamuru mshtakiwa kurudishwa rumande hadi hapo dhamana yake itakapokamilika. Kesi hiyo itatajwa tena Februari 11 mwaka huu.

Mwisho

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni