.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 23 Januari 2015

MWILI WA MFALME WA SAUDI ARABIA WAINGIZWA MSIKITINI KUANZA TARATIBU ZA MAZISHI

Mwili wa mfalme wa Saudi Arabia Abdullah bin Abdulaziz umebebwa na kuingizwa katika msikiti uliopo Riyadh, leo majira ya mchana, ikiwa ni chini ya saa 24 baada ya kufariki dunia.

Mwili huyo ulikuwa umevingirishwa kwenye kitambaa, wakati ukiingizwa kwenye msikiti mkubwa wa Riyadh wa Turki Bin Abdullah ukiwa kwenye machela.

Mfalme huyo alifariki usiku wa kumkia leo akiwa na umri wa miaka 90, akisumbuliwa na nimonia, atazikwa kwenye kaburi lisilo na alama hii leo, kulingana na tamaduni za Kiislam.

Taifa la Saudi Arabia lipo katika maombolezo, huku makumi kwa maelfu ya watu wakikusanyika Jijini Riayadh na Mecca kutoa heshima zao za mwisho.
             Mwili wa mfalme wa Saudi Arabia Abdullah bin Abdulaziz ukiingizwa msikitini

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni