Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi wa mamlaka ya maji Njombe ndugu Daudi Majani.
Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla akibadilishana mawazo na mkuu wa mkoa Njombe, Dr Rehema Nchimbi.
Akikagua kazi uunganishaji na ulazaji mabomba eneo la Airport Njombe.
Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla akipata maelezo ya chanzo cha maji cha Hagafilo kutoka kwa mdau wamazingira na mlezi wa Walei ndugu Edwin Kilasi.
Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla ametembelea mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Njombe (NJUWASA) na kutembelea vyanzo vya maji vya Magoda,Hagafilo,Njenga na Kibena.
Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla ametembelea mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Njombe (NJUWASA) na kutembelea vyanzo vya maji vya Magoda,Hagafilo,Njenga na Kibena.
Katika ziara hiyo, Mh Makalla amekagua ujenzi wa mradi wa kuboresha maji mji wa Njombe kuanzia kwenye chanzo cha Mto Njenga, ulazaji mabomba na matanki makubwa 3.
Mradi wa Njenga utagharimu sh 3.5bilioni na tayari umeshagharimu sh 2.2 bilioni na utakamilika mapema machi na kuongeza upataikanaji maji kutoka asilimia 43 hadi asilimia 79.
Mh Makalla amewataka wakandarasi wote wa mradi huu kuanzia chanzo, mabomba na matanki wakamilishe na mapema machi wananchi mji Njombe wapate maji ya uhakika. Aidha amefanya mkutano na wadau wote wa maji mji wa Njombe
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni