Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa nchini Tanzania (PCCB), leo imewafikisha katika mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, watumishi wawili
waaandamizi wa umma kwa tuhuma za kuhusika na rushwa katika sakata la
ufisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow.
Watuhumiwa hao ni pamoja na
aliyekuwa Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Bw. Teophil John, anayetuhumiwa kupokea fedha za
Tanzania shilingi milioni 161.4 kutoka kwa mfanyabiashara Bw. James
Rugemarila, fedha zinazodaiwa kuwa zilitolewa katika mazingira ya
rushwa.
Mtuhumiwa mwingine ni Bw. Rugonzibwa
Teophil ambaye ni Mhandisi Mwandamizi kutoka Wakala wa Nishati
Vijijini (REA), ambaye kwa mujibu wa hati ya mashtaka, yeye
anatuhumiwa kupokea fedha shilingi milioni 323, kutoka kwa Bw. James
Rugemarila pia katika mazingira yanayodhaniwa kuwa ni ya rushwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni