.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 16 Januari 2015

SAKATA LA ESCROW VIGOGO WENGINE WATATU WAPANDISHWA KIZIMBANI


Maafisa watatu mmoja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Mamlaka ya Mapato (TRA) pamoja na wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) wamefikishwa leo Mahakamani Hakimu Mkazi Kisutu kuhusina kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow.

Waliofikishwa mahamama hiyo leo Jiji Dar es Salaam, Mwanasheria wa Tanesco Stephen Urassa, Afisa Misamaha ya Kodi TRA Kyabukoba Mutabingwa na Mkurugenzi wa Fedha BOT Julius Angelo, ambao wote wanatuhumiwa kuchukua rushwa ya fedha za akaunti ya Escrow.

Katika kesi hiyo iliyoletwa na Taasisi ya Kusuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) Urasa anashtakiwa kwa kuchukua rushwa ya shilingi milioni 161.7, Angelo anashtakiwa kuchukua rushwa ya shilingi milioni 161.7 na Mutabingwa kwa kupokea shilingi bilioni moja na laki sita.

Mtuhumiwa Stephen Urassa ametoka nje kwa dhamana wakati wenzake Kyabukoba Mutabingwa na Julius Angelo wamepelekwa rumande baada ya kushindwa masharti ya dhamana.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni