Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe
amesema video mpya ya Dola ya Kiislam (IS) inayotishia kumuua mateka
Kenji Goto ndani ya saa 24, inapaswa kulaaniwa na kukemewa.
Katika picha ya video sauti
inayoaminika kuwa ni ya Goto raia wa Japan, inasikika ikisema yeye na
rubani wa Jordan, watauwawa iwapo Jordan haitomuachia mwanamke wa
Irak aliyehukumiwa kifo.
Bw. Abe amesema nchi ya Japan
inashirikiana na nchi ya Jordan ili kufanikishwa kuachiwa kwa raia
hao wao wawili.
Siku ya jumapili IS ilisema imemua
raia mwingine wa Japan, Haruna Yukawa, baada ya dai lau la kupatiwa
dola milioni 200, ili wamuachie kushindikana.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni