.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 16 Februari 2015

MAMIA YA WAOMBOLEZAJI WASHIRIKI MAZIKO YA MKE WA JOHN KITIME HII LEO

Umati wa waombolezaji ulioshiriki kwenye mazishi ya Mke wa Mwanamuziki Mkongwe hapa nchini,Bw. John Kitime,Marehemu Janeth Joan Chidosa Kitime alizikwa leo kwenye makaburi ya Kinondoni,jijini Dar es salaam.
Taratibu za mazishi zikiendelea kwenye makaburi ya Kinondoni,jijini Dar es salaam leo.
Mume wa Marehemu Janeth Joan Chidosa Kitime,Bw. John Kitime akitoka kuweka shada la maua kwenye kaburi la mkewe wakati wa mazishi yaliyofanyika jioni hii kwenye makaburi ya Kinondoni,jijini Dar es salaam.
Watoto wa Marehemu wakielekea kuweka shada la maua kwenye kaburi la Mama yao.
Mfiwa Bw. John Kitime katikati akiwa na Watoto zake mara baada ya Mazishi kwenye makaburi ya Kinondoni,jijini Dar es salaam.
Wadau mbalimbali wakimfariji mfiwa,Mzee John Kitime mara baada ya mazishi kwenye makaburi ya Kinondoni,jijini Dar es salaam leo.
Dada Nyota Waziri akimfariji Bw. John Kitime mara baada ya mazishi ya mkewe kwenye makaburi ya Kinondoni,jijini Dar es salaam.
                                                 Anko Kidevu akimfariji rafiki yake Bw. John Kitime.
Baadhi ya Wanachama wa TBN waliowakilisha kwenye mazishi ya mke wa mwanachama mwenzao,Bw. John Kitime kwenye makaburi ya Kinondoni,jijini Dar es salaam leo.kutoka kulia ni Cathbert Kajuna,Mkala Fundikira,Jennifer Livgha a.k.a ChingaOne,Ahman na Othman Michuzi pamoja na Muhidin Sufiani. Picha kwa hisani ya Mtaa kwa Mtaa Blog

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni