Mwanariadha wakike raia wa Kenya
Hyvon Ngetich ameushangaza ulimwengu kwa ushujaa alioonyesha kwa
kumaliza mbio za marathoni za Austin zilizofanyika Texas akitambaa na
kushika nafasi ya tatu.
Hyvon Ngetich aliishiwa nguvu akiwa
umbali wa mita 400 kabla ya kumaliza mbio hizo na kuanguka
alipojaribu kunyanyuka akashindwa na kuamua kutambaa hadi akamaliza
mbio hizo, huku akikataa msaada wa kubebwa kwenye kiti cha magurudumu
ili atolewe nje.
Kwa kuonyesha ushujaa huo Ngetich
alipewa zawadi ya fedha sawa na mshindi wa pili, na baada ya hapo
alikimbizwa hospitali kutibiwa majeraha ya magoti na alikutwa na
ugonjwa kisukari cha chini.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni