Naibu Waziri wa Maji Amos Makalla leo ameendelea na ziara yake mkoa wa Kilimanjaro, na leo alikuwa wilaya ya Mwanga .
Katika ziara ya leo ameongea na uongozi wa wilaya ya Mwanga, amekagua miradi ya maji vijiji vya Kisanjini, Msangeni na Lomwe.
Pia amekagua maandalizi ya vifaa na eneo patakapojengwa mradi mkubwa wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe utakapgharimu dola za kimarekani milioni 41.5
Akiongea na wananchi kijiji cha Njiapanda unapojengwa mradi, Mh Makalaa amesema amefurahishwa na mkandarasi kuanza kazi na amewataka waanchi kutoa ushirikiano na wawe waaminifu kwa wale watakaopata ajira.
Mradi huo utachukua miezi 31 na utaufaisha vijiji 17 vya wilaya ya Same, vijiji 16 vya wilaya ya Mwanga na vijiji 5 vya wilaya ya Korogwe.
Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla akizindua mradi maji kijiji cha Kisanjini kwa kumtwisha mama ndoo ya maji.
Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makalla akiongea na mr Sharif Salah mhandisi mshauri wa mradi wa Same-Mwanga-Korogwe.
Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla akikagua mradi huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni