Mfuko wa penseni wa PSPF ulipata fursa ya kukutana na kutoa elimu kuhusu huduma mbalimbali wanazo zitoa na kuweza kuwapa maelezo ya baadhi ya mafao yanayo tolewa kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa (PSS) kwa Askari na watumishi raia makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dae es Salaam.
Bi. Matilda A. Nyallu ambaye ni Afisa MatekelezoMwandamizi(SCO) wa mfuko wa PSPF aliweza kutoa rai kwa Askari na watumishi raia wote waweze kujiunga na mfuko wa jamii wa PSPF ili kuweza kupata mafanikiona kunufaika.
Pia alitoa mifano michache kwa ambao watajiunga na mfuko huo ambapo kwa Askari na watumishi raia alitaja kuwa wanaweza kupata mikopo ya kuanzia maisha ambayo itakuwezesha kupata nyumba ambazo wamezijenga kwa ajiri ya mtanzania aweze kununua au kukopeshwa na baadae kuweza kurejesha mkopo huo wa nyumba, pia aliongeza kwa kusema nyumba zote zimewekewa bima endapo tatizo lolote likitokea basi nyumba hizo zitakuwa salama.
Hata hivyo afisa wa mfuko wa Pensheni Bw.hadji Jamadary aliweza kuwaasa na kuwasisitiza mambo mbalimbali yanoyo tekelezwa na mfuko na kuwataka wawe miongoni mwa watu wenye muamko wa kujiunga ili wengine waweze kuiga mfano kutoka kwao.
Mfuko wa pensheni ni mfuko wa kijamii unao toa huduma na kukidhi mahitaji ya jamii paspo na gharama zinazo iumiza jamii , kujiunga na mfuko wa PSPF ndiko kutakako kuokoa katika kukuwekea dhamana ya maisha yako iwe ni katika elimu ,makazi,ugonjwa na hata ujasiliamali .
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni