.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 14 Machi 2015

WAZIRI CHIKAWE AKABIDHI PIKIPIKI 35 KWA MAKATIBU KATA WA CCM WILAYA YA NACHINGWEA LEO

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (wapili kushoto) akimkabidhi kadi ya pikipiki Mwenyekiti wa Makatibu Kata wa CCM Wilaya ya Nachingwea, Ally Napepa. Waziri Chikawe alikabidhi pikipiki 35 kwa makatibu kata wilayani humo kwa ajili kazi ya uendeshaji wa shughuli za chama ikiwemo kuwahamasisha wananchi katika kata zao kujiandisha ili kuipigia kura ya ndiyo Katiba iliyopendekwa na Bunge, pamoja na kujiandaa na uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu. Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za CCM wilayani humo. Kulia ni Katibu wa CCM wilaya hiyo, Mussa Liliyo. Picha na Felix Mwagara.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kulia) akiwasisitiza Makatibu Kata wa CCM Wilaya ya Nachingwea, kuzitumia kwa uangalifu pikipiki 35 alizowakabidhi kwa ajili ya kazi za uendeshaji wa shughuli za chama ikiwemo kuwahamasisha wananchi katika kata zao kujiandisha ili kuipigia kura ya ndiyo Katiba iliyopendekwa na Bunge, pamoja na kujiandaa na uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu. Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za CCM wilayani humo. Picha zote na Felix Mwagara.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni