.
.
.
.
.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga
|
TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.
mbani
NYUMBANI
HABARI
SIASA
MICHEZO
BURUDANI
TABASAMU
KIMATAIFA
Jumatatu, 20 Julai 2015
DKT JOHN POMBE MAGUFULI ATIKISA JIMBONI KWAKE CHATO,WANANCHI WAIBUA SHANGWE KILA KONA YA MJI
Mbunge wa Chato na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa mji huo waliojitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo akitokea mkoani Mwanza ambako nako alipita kujitambulisha na kuwashukuru wakazi wa jiji hilo ambao nao walijitokeza kwa wingi. Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli ndani ya mji wa Chato kuliibuka shamra shamra za mapokezi zilizokuwa zikirindima kila pande wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli.
Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Chato na vitongoji vyake waliokuwa
wamekusanyika kwenye kituo cha mabasi wilayani humo wakishangilia kwa
furaha kubwa mara baada ya Mbunge wao na Mgombea Urais kwa chama cha
Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli kujitambulisha kwao.
Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Chato na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumlaki Mbunge wao na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo na shamra shamra za mapokezi kurindima kila kona wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli,huku wengine wakiwa wamebeba mabango kama hivyo pichani.
Mbunge wa Chato na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa mji huo waliojitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo akitokea mkoani Mwanza ambako nako alipita kujitambulisha na kuwashukuru wakazi
wa jiji hilo ambao nao walijitokeza kwa wingi. Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli ndani ya mji wa Chato kuliibuka shamra shamra za mapokezi zilizokuwa zikirindima kila pande wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Luhavi akiwasalimia wachama wa CCM pamoja na Wananchi waliofika kumlaki Dkt Magufuli jioni ya leo katika kituo cha mabasi cha zamani ndani ya wilaya hiyo.
Ilikuwa ni shangwe tu jioni ya leo ndani ya Wilaya ya Chato ambako ndiko nyumbani kwa Mbunge na
Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli.
Mwananchi akiwa amekumbwa na joto la furaha mara baada ya kumuona Dkt Jonh Magufuli akiwa na msafara mzima wakielekea jimboni kwake Chato mkoani Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh.Magesse Mulongo akiwasalimia wananchi wa Chato jioni ya leo,kabla ya kumkaribisha Dkt John Magufuli aliyewasili mjini
humo jioni ya leo akitokea mkoani Mwanza akijitambulisha kwa wananchi na
kuwashukuru.
Dkt Magufuli akizungumza jambo kwa maelfu ya wakazi wa mji wa Chato jioni ya leo.
Dkt Magufuli akifurahia jambo mbele ya umati wa watu,mara baada ya kujitambulisha kwao.
Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwashukuru wakazi wa mji huo kwa kujitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo akitokea mkoani Mwanza ambako nako alipita kujitambulisha na kuwashukuru wakazi wa jiji hilo ambao nao walijitokeza kwa wingi. Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli ndani ya mji wa Chato kuliibuka shamra shamra za mapokezi zilizokuwa zikirindima kila pande wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli.
Maelfu ya Watu walijitokeza kumlaki Dkt Magufuli jioni ya leo mjini Chato
Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga Wananchi wa Chato waliojitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kumaliza kujitambulisha na kuwashukuru kwa kiasi kikubwa kwa kuchaguliwa kwake katika nafasi ya kupeperusha bendera ya chama chake kuwania nafasi ya Urais .PICHA NA MICHUZI JR-CHATO-GEITA.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni
Chapisho Jipya
Taarifa za zamani
Nyumbani
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni ( Atom )
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni