‘Makala ya Kusisimua yenye matukio yenye hisia nzito.’
Andy Markowitz, Tovuti ya Muziki wa Filamu Music Film Web
‘Tafakari ya kusisimua ya urafiki usio wa kawaida kati ya Kijana Mtengenezaji wa filamu na diva wa Zanzibar mzee wa miaka 100 Zanzibar diva’ Garth Cartwright - mwandishi, “More Miles Than Money”Umbali mkubwa kuliko fedha”
‘Uwasilishaji wa wa nyota …iliyofifia na kuifanya ing’are upya’
Martin Mhando, Mkurugenzi ZIFF
Nilimpiga Picha Bi Kidude “I Shot Bi Kidude”, ni makala mpya ya simulizi iliyotayarishwa na Andy Jones, mtengenezaji wa filamu wa Uingereza ambayo itahitimisha Tamasha la Filamu la Kimataifa hapa Zanzibar,. Watazamaji wa Zanzibar watamsikia msimulizi mwenyewe akisimulia kwa lugha ya Kiswahili ambayo alijifunza kwa muda mfupi matamshi kwa msaada wa wanamziki Wazanzibari Mim Suleiman na Bwana Mohammed Issa Matona.
Kwa kipindi cha zaidi ya miaka minne, kuanzia 2003 mpaka 2006, Andy Jones alimfuata Bi Kidude alipokuwa akisafiri duniani.
Matokeo yake ni kupokea tuzo ya filamu AS OLD AS MY TONGUE, ambayo ilionyeshwa kwa mara ya kwanza katika mwaka 2006 na baadaye iliendelea kuwa kivutio kwenye matamasha ya filamu na muziki duniani kote..
Baada ya kutembelea Zanzibar kila mwaka kwa karibu muongo mmoja, Jones hakuweza tena kumuona Bi Kidude kwa muda wa miaka mitatu.
Katika mwezi Agosti mwaka 2012, taarifa zilifika Uingereza zikieleza kuwa mwanamziki kinara maarufu Africa Mashariki ametekwa nyara . Haikuchukua muda mrefu Andy alirudi Zanzibar kupata ukweli wa taarifa .
Wiki chache tu baada ya kisa hicho kuibuliwa kwa picha zilizopigwa na Natalie Haarhoff kutoka Afrika ya Kusini , muimbaji mzee sana wa kimataifa amefariki, akiwa na umri unaosemekana kuwa zaidi ya miaka mia moja .
Wiki chache tu baada ya kisa hicho kuibuliwa kwa picha zilizopigwa na Natalie Haarhoff kutoka Afrika ya Kusini , muimbaji mzee sana wa kimataifa amefariki, akiwa na umri unaosemekana kuwa zaidi ya miaka mia moja .
Jones alikurupuka kutoka nyumbani kwake huko Newcastlena kufika uwanja wa ndege wa Heathrow dadikia chache kabla ya ndege iliyopangwa kwenda Nairobi kuondoka.
Alifika kwenye mazishi ambayo yalishtua kisiwa kizima..“I SHOT BI KIDUDE, ni simulizi yangu kuhusu mambo yalivyokuwa wakati wa mwisho wa maisha ya Bi Kidude’ .
Kama ilivyo kwenye simulizi nyingine , kuna maelezo mbalimbali kuhusu ukweli wa jambo. Kimsingi kuna vitu vingine ambavo si rahisi kwa mgeni kuvitambua, hata hivyo ninatumaini kuna vitu vingine haviwezi kufichika machoni .
Ninaloona mimi hisia ya kusherehekea nguvu za muziki na kufanya vitu ambavyo vinatuletea furaha pale tunapoweza ” Andy Jones anasema.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni