Mbunge wa jimbo la Kahama mkoani Shinyanga, Mh James Lembeli ametangaza rasmi kujivua uanachama wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema ) kuanzia leo.
Mh Lembeli ametangaza uamuzi huo muda mfupi uliopita mbele ya waandishi wa habari, Blue Pearl Hotel jijini Dar es Salaam.
Akielezea sababu za kuondoka CCM na kujiunga na Chadema, Mh Lembeli amesema mizengwe aliyokuwa akifanyiwa na viongozi wa chama hicho mkoa wa Shinyanga tangu uchaguzi uliopita wa mwaka 2010 ndio sababu kubwa ya yeye kukimbilia upinzani.
Katika hatua nyingine Mh Lembeli amesema katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2015, atagombea Ubunge wa jimbo la Kahama mjini kwa tiketi ya Chadema na kuwaomba wananchi kumuunga mkono.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni