Jeshi la polisi Jijini Dar es
Salaam, limesema limefanikiwa kuwakamata majambazi watano wanaodaiwa
kuhusika na tukio la uvamizi katika kituo cha polisi cha Stakishari
kilichopo Ukonga.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya
Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema majambazi hayo yamekamatwa
maeneo ya Mbagala ambapo katika tukio hilo wamekamata pia fedha kiasi
cha shilingi milioni 170 na bunduki 16 miongoni mwao ni zile
zilizoibiwa katika kituo cha Stakishari.
Vilevile Kamanda Kova amesema kuwa
bado wanawatafuta watu kadhaa wanaotuhumiwa ni wafuasi wa genge hilo
hatari la uhalifu ambalo mbali kuvamia kituo cha Stakishari, genge
hilo pia linahusika na uporaji fedha katika taasisi mbalimbali za
fedha nchini.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni