Baadhi ya Viongozi, Wazee na Wananchi wa Jimbo la Kitope waliojumuika pamoja na Mbunge wao Balozi Seif Ali Iddi katika chakula cha mchana kusherehekea siku kuu ya iddi el fitri baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani hapo Ofisi ya Jimbo Kinduni.
Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Baadhi ya Viongozi, Wazee na Wananchi wa Jimbo hilo kabla ya kula nao pamoja chakula cha mchana kusherehekea siku kuu ya Iddi el fitri.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Jimbo la Kitope Mzee Suleiman Thabit akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wenzake mara baada ya kula pamoja chakula cha mchana na Mbunge wao wa Jimbo hilo Balozi Seif Ali Iddi.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi alisema Waumini wa Dini ya Kiislamu pamoja na Wananchi wanapaswa waendelee kushikamana katika kudumisha amani ili hazina hii iliyoipatia sifa Tanzania katika Nyanja ya Kimataifa izidi kung’ara.
Alisema suala la amani ambalo ndio msingi mkuu wa utulivu wa Jamii popote pale Duniani imesisitizwa na kuagizwa isimamiwe ipasavyo hata katika maamrisho ya Dini na Vitabu vyake.
Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitoa nasaha hizo katika hafla ya kutoa mkono wa iddi wakati akizungumza na Viongozi pamoja na Wananchi wa Matawi,Wadi na Jimbo la Kitope alipokula nao pamoja chakula cha mchana hapo Ofisi ya Jimbo Kinduni Wilaya ya Kaskazini “B”.
Alisema suala la amani ambalo ndio msingi mkuu wa utulivu wa Jamii popote pale Duniani imesisitizwa na kuagizwa isimamiwe ipasavyo hata katika maamrisho ya Dini na Vitabu vyake.
Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitoa nasaha hizo katika hafla ya kutoa mkono wa iddi wakati akizungumza na Viongozi pamoja na Wananchi wa Matawi,Wadi na Jimbo la Kitope alipokula nao pamoja chakula cha mchana hapo Ofisi ya Jimbo Kinduni Wilaya ya Kaskazini “B”.
Huo ni utaratibualiouandaa Balozi Seif kwa takriban miaka mitatu sasa wa kula na wananchi wa Jimbo lake chakula cha Mchana kusherehekea siku kuu ya Iddi el – Fitri baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Balozi Seif alisema maamrisho ya Dini pamoja na vitabu vyake yamekuwa yakielekeza umuhimu wa kuwepuka mifarakano na pale inapotokea kwa bahati mbaya waumini na wana jamii hao wanapaswa kurejea katika vitabu vya Dini.
Amewakumbusha Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kumaliza funga sita iliyosuniwa ili wapate fadhila kubwa ambazo Muumini huzipata kama aliyefunga ramadhani mwaka mzima.
Balozi Seif Ali Iddi alitumia fursa hiyo kuwaaga rasmi wananchi na wana CCM wa Wadi ya Upenja ambayo pamoja na Matawi yake kwa sasa imeunganishwa katika Jimbo Jipya la Kiwengwa kufuatia mabadiliko ya majimbo yaliyofanywa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar hivi karibuni.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Viongozi na Wananchi hao wa Jimbo la Kitope Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Kitope Mzee Suleiman Thabit aliwakumbusha Wananchi na hasa Vijana kufahamu kwamba Mapinduzi Daima yataendelea kuimarika siku hadi siku.
Mzee Thabit alisema Uimarishaji huo umelenga zaidi katika mfumo unaoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa uimarishaji wa maendeleo na kustawisha Jamii.
Mwenyekiti huyo wa Baraza la Wazee la Kitope alimpongeza Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope Balozi Seif kwa juhudi alizozichukuwa za kulijengea miundo mbinu imara na kuliacha eneo hilo katikia maendeleo makubwa ya kupigiwa mfano.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni