.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 21 Julai 2015

MAMA SALMA KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA 9 WA WAKE WA MARAIS KUHUSU KANSA HUKO NAIROBI.

1
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akielekea kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Jomo Kenyetta huko Nairobi kuhudhuria mkutano wa 9 wa Wake wa Marais wa Nchi za Afrika unaozungumzia magonjwa ya saratani ya matiti, shingo ya kizazi na tezi dume tarehe 20.7.2015. PICHA ZOTE NA JOHN LUKUWI
3
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mke wa Rais wa Niger Madame Dkt. Lalla Malika Issofou Mahammadou wakiwa kwenye sherehe za ufunguzi wa mkutano wa 9 wa Wake wa Marais wa nchi za Afrika. Mkutano huo ulifunguliwa rasmi na Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyetta (hayupo pichani) tarehe 20.7.2015.
4
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na wake wa Marais kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wamesimama wakati wimbo wa Taifa wa Kenya ukiimbwa.
6
Baadhi ya Wake wa Marais wa Nchi za Afrika wakishiriki kumvisha mkanda maalum kwa kuteuliwa kwake kuwa Balozi wa Hiari kwenye Masuala ya Afya ya Mama na Mtoto Barani Afrika. Wanaomvisha mkanda huo kwa niaba ya wake wa Marais ni (kutoka kushoto kwenda kulia) Princess Nikky Onyeri, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa ‘Forum of African First Ladies against Cervical, Breast and Prostate Cancer, Mama Dkt. Lalla Mahammadou wa Niger, Mama Monica Geingos wa Namibia, Mama Mary Ayen Mayardit wa Sudan Kusini. Mama Salma Kikwete na Mwisho ni Mama Mathato Mosisili wa Lesotho.

5
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akiwa amesimama na baadhi ya wake wa Marais wa Afrika wakati wimbo wa Mataifa ya Afrika ukiimbwa. Kushoto kwa Rais Kenyatta ni Mkewe Mama Margret Kenyatta akifuatiwa na Mke wa Rais wa Namibia Mama Monica Geingos, Mama Salma Kikwete na mwisho ni Mama Dkt. Lalla Malika Issofou Mahammadou wa Niger.
2
Baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania wanaoshiriki kwenye mkutano wa 9 wa Wake wa Marais wa Afrika wakifuatilia kwa makini sherehe za ufunguzi.
     7
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiteta jambo na Princess Nikky Onyeri, Mwanzilishi wa Forum of African First Ladies Against Cervical, Breast and Prostate cancer mara baada ya viongozi hao kutembelea Hospitali ya HH Aga Khan jijini Nairobi tarehe 20.7.2015.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni