Baraza la Seneti limesema serikali
ya Kenya ilimtelekeza muigizaji mkongwe na maarufu Mzee Ojwang'
aliyechangia katika kuhamasisha umoja miongoni mwa wakenya, akifariki
dunia akiwa masikini.
Wakijadili Muswada wa Kutambua Watu
Waliofanikiwa kwa Mchango wao kwa Taifa, Maseneta wamesema ilikuwa ni
kosa kumuacha Mzee Ojwang' kufariki dunia bila kutambuliwa mchango
wake na Ikulu.
Maseneta hao wameikosoa serikali ya
Kenya kwa kungojea mashujaa wa taifa wafe kwanza ndipo waanze
kuwapongeza kwa mambo makubwa waliyolifanyia taifa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni