Rais wa Shirikisho la Soka Duniani
(FIFA) aliyenakashfa Sepp Blatter amejikuta akirushiwa rundo la dola
feki na mchekeshaji ambaye alizamia mkutano wake uliofanyika huko
Zurich hii leo.
Mchekeshaji huyo Muingereza Simon
Brodkin aka Lee Nelson, aliingia kwa utulivu hadi alipokaa Blatter na
kuanza kumrushia dola huku akisema hizi ni za kwa ajili Korea
Kaskazini mwaka 2026.
Baada ya kufanya hivyo akimaanisha
kuwa ni hongo ya Korea Kaskazini kuanda michuano ya dunia,
mchekeshaji huyo aligeukia vyombo vya habari na kuongea navyo huku
Blatter akiwaita walinzi kwa kutumia mikono ili wamuondoe.
Jiandae kupokea hongo kutoka Korea Kaskazini
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni