Shushu mmoja mwajiriwa wa Shirika la
Taifa la Ujasusi la Korea Kusini, amekutwa akiwa amekufa ndani ya
gari lake ikiaminika kuwa amejiua, polisi wamesema.
Kifo cha shushu huyo aliyejiua
kwenye barabara iliyo juu ya kilima, kimetokea wakati kukiibuka kwa
kasi kashfa ya udukuzi wa maongezi ya simu.
Mtu huyo mwaname ameacha ujumbe wa
kukiri kujiua na kusema amefuta taarifa muhimu kuhusiana na udukuzi
wa simu.
Ilibainika kuwa simu za kinganjani
zilikuwa zinafuatiliwa na majashusi wa Korea Kusini, kabla ya
uchaguzi wa urais wa mwaka 2012.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni