.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 14 Agosti 2015

JESHI LA POLISI NCHINI LAPIGA MARUFUKU MISAFARA YA KWENDA KUCHUKUA FOMU NEC PAMOJA NA KUSAKA WADHAMINI


                                                                               Na Lorietha Laurence –Maelezo. 

Jeshi la Polisi nchini limesitisha maandamano ya wafuasi wa vyama vya siasa wakati wa kuchukua ,kutafuta wadhamini, na kurejesha fomu za kugombea nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Naibu Inspekta Jenerali wa jeshi la Polisi Abdulrahman Kaniki amesema kuwa jeshi limechukua hatua hiyo kutokana na ukiaukwaji wa sheria za usalama barabarani uliojitokeza wakati wagombea wa vyama vya CHADEMA na CCM walipochukua fomu za kugombea Urais makao makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

“Kwa sababu za kiusalama Jeshi la Polisi linasitisha maandamano ya aina yoyote wakati wote wa zoezi la kuchukua fomu, kutafuta wadhamini mikoani pamoja na zoezi la kurejesha fomu “ alisema Kaniki.

Aidha aliongeza kuwa jeshi la Polisi nchini linafanya utaratibu wa kuwakutanisha wadau wote wa siasa ikiwemo viongozi wa vyama vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi Mkuu ili kuona namna bora ya kufanya uchaguzi katika hali ya amani na utulivu.

“Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua za kisheria mgombea, kiongozi, mfuasi au chama chochote cha siasa kitakachokiuka agizo hili,” alisema.

Hatua hiyo ya jeshi la Polisi nchini inatokana na baadhi ya wagombea wa nafasi za Urais kufuatana na kundi kubwa la wanachama, na wapambe wao wakati wa kuchukua fomu za kuomba kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi hivi karibuni na kuhatarisha usalama ikiwemo kufungwa kwa barabara na kusababisha baadhi ya shughuli za kijamii kusimama.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni