Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Frolence Turuka amesema hayo leo alipo itembelea Tume ya Tafifa ya Uchaguzi kuona maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ambapo alishuhudia vifaa mbalimbali vya Uchaguzi vikiwasili na Kupokelewa katika ofisi ya NEC kitengo cha Daftari Bohari.
"Changamoto ya kifedha ambayo Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilikuwa ikikabiliana nayo awali sasa haipo tena kwakuwa serikali imedhamiria kuipa NEC fedha zote ambazo inazihitaji katika kuhakikisha Uchaguzi mkuu unafanyika Octoba 25 mwaka huu.
Fedha hizo zitatolewa kwa awamu, kutokana na ratiba ya tume ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vifaa ambavyo vimeanza kuwasili , mafunzo kwa wasimamizi wa Uchaguzi na zoezi zima la Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais.
Vifaa vilivyo wasili Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni pamoja na vitutuli[vibanda vya kupigia kura], mabango [yanayo onesha kituo cha kupigia kura.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni