Shirikisho la Mpira Miguu nchini (TFF), limetuma salamu za rambirambi kwa familia za Lubawa, kufutia kifo cha mwamuzi mstaafu na kamishina wa TFF Saleh Lubawa kilichotokea jana jioni.
Katika salam zake kwenda kwa familia ya marehemu, TFF imesema inawapa pole wafiwa, ndugu jamaa na marafiki na kwa niaba ya familia ya mpira miguu nchini wapo pamoja na familia katika kipindi hichi cha maombolezo.
Mazishi ya marehemu Saleh Lubawa yanatarajiwa kufanyika leo jioni nyumbani kwake eneo la Kongowe – Kibaha.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni