Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr. Fenella Mkangara leo Jumapili, Septemba 13, 2015 saa 8 kamili mchana anatarajiwa kuzindua rasmi fainali za michuano ya Airtel Rising Star katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Jumla ya timu sita zinatarajiwa kushiriki michuano hiyo ambayo imekua ikifanyika kila mwaka nchini kwa udhamini wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, ambapo vijana wenye vipaji huchaguliwa na kupata nafasi ya kujiunga na vituo vya michezo (Academy) za Dakara – Senegal na Doha – Qutar zinazomilikiwa na kampuni hiyo.
Katika uzinduzi huo wa leo, timu za mkoa wa Ilala, Kinondoni, Mbeya, Morogoro, Mwanza na Temeke zinatarajiwa kupambana kusaka mshindi kwa fainali hizo za kitaifa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni